Nyati aua watu watatu Mtwara
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo
Muktasari:
- Watu watatu wakazi wa kijiji cha Mahurunga wilayani Mtwara wamefariki baada ya kushambuliwa na nyati wakiwa shambani.
Mtwara. Watu watatu wakazi wa kijiji cha Mahurunga wilayani Mtwara wamefariki baada ya kushambuliwa na nyati wakiwa shambani.
Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amewaeleza waandishi wa habari leo Alhamisi Machi 24, 2022 kuwa tukio hilo limetokea Machi 20 saa 5 asubuhi wakati watu hao wakiwa shambani.
Amewataja watu hao kuwa ni Rashid Bakari (40) mkazi wa kijiji cha Kitunguli, Salum Yusuf (46) na Said Musa (45) wakazi wa kijiji cha Mahurunga.
Baada ya kushambulia taarifa zilifika kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaolinda mpaka ambao walifika haraka na kumuua.
Baada ya uchunguzi miili Ilichukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi na kuwataka wananchi kutoa taarifa wanapoona wanyamapori katika makazi ya watu.