Ole Sendeka ataka soko la Tanzanite Mirerani

Ole Sendeka ataka soko la Tanzanite Mirerani

Muktasari:

  • Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka amemuomba Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa biashara ya madini ya Tanzanite ifanyike eneo la Mirerani ili kukuza uchumi wa eneo hilo.

Mirerani. Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka amemuomba Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa biashara ya madini ya Tanzanite ifanyike eneo la Mirerani ili kukuza uchumi wa eneo hilo.

Ole Sendeka ameyasema hayo leo Jumatano Julai 7, 2021 katika mji mdogo wa Mirerani wakati Majaliwa akizindua kituo cha Tanzanite Magufuli.

Amesema soko la madini ya Tanzanite likianzishwa Mirerani uchumi wa wananchi utapanda na kutaka biashara hiyo kutofanyika eneo jingine.

Amesema madini hayo yapo Mirerani ila wananchi wake wanaishi maisha ya shida," pamoja na elimu ya kutotorosha madini kutolewa wananchi wanaelewa ila upekuzi wa staha unapaswa kufanywa.”

Pia ameomba eneo la mamlaka ya biashara ya nje EPZA ambapo kuna sehemu imetengwa ikiwemo barabara ya lami ianze kutumika, “tunaomba pia barabara ya lami kutoka nje ya ukuta iungane na barabara kuu ya Kia-Mirerani kwani ni umbali mdogo kutoka kwenye ukuta.”