Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ole Sendeka: Waungeni mkono waliochaguliwa, hata kama mliwapinga

Mbunge wa zamani wa Simanjiro, mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka (katikati) akizungumza kwenye kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai katika sherehe ya kuvuka rika kwa watoto wa mdau wa maendeleo Siria Makuruza kwa kuiasa jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi walichaguliwa. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Jamii imetakiwa kuwaunga mkono viongozi waliochaguliwa wakiwemo madiwani na mbunge hata kawa hawakuwa chaguo lao kwani ni viongozi wanaowaongoza hivi sasa.

Simanjiro. Mbunge wa zamani wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, amewataka wananchi kuwapa ushirikiano viongozi waliochaguliwa kuwaongoza, hata kama hawakuwaunga mkono awali.

Ole Sendeka ameyasema hayo, leo Jumapili, Julai 19, 2026 katika Kijiji cha Naepo, wilayani Simanjiro, wakati wa sherehe za kuvuka rika kwa watoto wa mdau wa maendeleo, Siria Makuruza.

Amesema ni vema jamii ikatoa ushirikiano kwa wabunge na madiwani waliochaguliwa, hata kama kipindi cha kampeni hawakuwaunga mkono.

"Hivi sasa uchaguzi umeshapita, tumeshapata wabunge na madiwani, hivyo tuwaunge mkono kwa ajili ya kufanikisha maendeleo hata kama hatukuwaunga mkono awali."

"Tuweke rekodi sawa, mimi sikushindwa ubunge Simanjiro ila jina langu lilibaki Dodoma kwa heshima halikurudishwa ila uchaguzi umeshapita tugange yajayo," amesema Ole Sendeka.

Miongoni mwa majina yaliyorudi kupigiwa kura za maoni ndani ya CCM ni la James Ole Millya ambaye aiibuka mshindi. 

Vikao vya juu vya CCM vilimteua Millya kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na kushinda na sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Simanjiro, Wambura Igembya, ameiasa jamii kuienzi na kuitunza tunu ya amani kwani ikitoweka kuipata tena ni kazi kubwa.

"Hapa kwenye sherehe tumekula nyama kwa amani na upendo ila kungekosekana amani tusingeweza kukaa pamoja kwa furaha na upendo hivi, hivyo tuitunze na tuihubiri amani," amesema.

Amewataka wana CCM kutowaunga mkono viongozi wanaotoa lugha za matusi kwenye majukwaa ya kisiasa.

"Viongozi wanapaswa kutoa maneno ya hekima na lugha za maendeleo siyo matusi jukwaani, mkiwaona msiwaunge mkono," amesema.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) usharika wa Purana, Sioni Abraham, amesema binadamu anapaswa kumrudia Mungu kipindi akiwa na nguvu na afya, siyo akikaribia kufa.

"Acheni kumrudia Mungu mkiwa mmechoka na kukaribia kufa, wakati wa kuwa na Mungu ni sasa ukiwa mzima na afya yako siyo ukiwa umechoka," amesema mchungaji Sioni.

Amesema hakuna mtu anatambua siku ya mwisho wake hivyo wanapaswa kurejea kwa Mungu kwa wakati huu ili wamtumikie wakiwa na nguvu na afya tele.