Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Osha yajikita kuwawezesha watu wenye ulemavu kupitia elimu ya usalama kazini

Ofisa Mafunzo wa Osha, Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu vihatarishi mahali pa kazi na udhibiti wake kwa wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB) katika semina ya mafunzo iliyoandaliwa na OSHA kwa kundi hilo.

Muktasari:

  • Elimu hiyo imetolewa kwa siku moja kwa wanachama 50 wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB) Dar es Salaam na Pwani.

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Osha, wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OshaKhadija Mwenda amesema taasisi hiyo inatambua thamani na mchango wa watu wenye ulemavu katika kujenga uchumi wa Taifa.

Amesema kutokana na umuhimu wa kundi hilo katika kujenga uchumi, Osha imekua ikiandaa mafunzo kwa ajili ya kundi hilo.

Mtendaji huyo ameyaeleza hayo leo Septemba 27,2025 Dar es  Salaam  wakati akifungua mafunzo kwa kundi la watu wasioona wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mafunzo yaliyolenga  kuliwezeshakundi hilo kushiriki shughuli za uzalishaji mali kwa kuzingatia kanuni bora za usalama na afya kazini.

Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yametolewa kwa wanachama 50 wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB) yamehusisha mada mbalimbali zikiwemo utambuzi na udhibiti wa vihatarishi vya usalama na afya pamoja na misingi ya huduma ya kwanza mahali pa kazi.

Mtendaji Mkuu wa Osha, Khadija Mwenda

Washiriki wa mafunzo hayo wanajihusisha na shughuli mbalimbali zikiwemo ushonaji, kilimo, ufugaji, uzalishaji wa bidhaa zikiwemo sabuni na biashara ndogondogo.

“Niwapongeze washiriki wote wa mafunzo kwa kuitikia mwaliko wa kushiriki mafunzo haya muhimu kwenu kwani ni dhahiri kuwa ulemavu ni hali tu ambayo haipaswi kuwa kikwazo kwenu kushiriki katika shughuli za kiuchumi,

“Sambamba na mafunzo haya, tutawapatia vifaa saidizi zikiwemo fimbo nyeupe, karatasi za nukta nundu pamoja na vitabu maalum vya nukta nundu vyenye maudhui ya mafunzo ya usalama na afya kwa ajili ya rejea zaidi.”amesema

Mwenda ameahidi mafunzo ya usalama na afya kwa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu yatafuatiwa na zoezi la kutembelea maeneo yao ya kazi kwa ajili ya kutathmini mazingira ya kazi ili kushauri namna sahihi ya kuboresha mazingira hayo.

Awali, akiwasilisha salamu za Jumuiya ya Wasiiona Tanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Omary Itambu, ameipongeza Osha kwakuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha watu wasioona pamoja na makundi mengine ya wenye ulemavu.

“Tunaiomba Osha kuendeleza utamaduni huu wa kutujali watu wenye ulemavu. Kwa niaba ya washiriki wenzangu niwahakikishie Osha kuwa mafunzo mliyotupatia si tu yatakwenda kuimarisha afya na usalama wetu bali yatatusaidia sana kuongeza thamani ya huduma na bidhaa tunazozalisha,” amesema.

 Itambu ametoa wito kwa washiriki wenzake wa mafunzo kuwa mabalozi wazuri wa Osha ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wenzao ambao hawakupata fursa ya kushiriki mafunzo.

Mratibu wa Idara ya Vijana wa Jumuiya ya Wasioona, Bakari Hassan, amesema jambo lililofanywa na Osha ni la kuigwa na Taasisi nyingine za kiserikali na zisizo za kiserikali, akisisitiza kwamba mafunzo hayo na vifaa saidizi walivyopewa vitarahisisha utendaji na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku.