Papa abadili sheria ya kanisa

Thursday January 14 2021
papapic

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis

By Mwandishi Wetu

Vatican. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amefanya marekebisho rasmi ya sheria ya kanisa hilo, ili kuruhusu wanawake kuchukua majukumu zaidi kinyume na ilivyokuwa hapo awali.

Sheria hiyo mpya kwa jina la Kilatini, Spiritus Domini au Roho ya Mungu inaruhusu wanawake kuhudumu kanisani kwa kusaidia makasisi. Hatua hiyo inaendana na ahadi aliyotoa awali ya kufanya marekebisho kwenye Kanisa Katoliki ambalo kihistoria limekuwa likihudumiwa na wanaume.

Sheria hiyo inasemekana kuwa itaimarisha zaidi msingi wa kanisa pamoja na kuhusisha kila mmoja kwenye shuguli za uinjilisti, ingawa Papa Francis alisema kuwa jukumu la kuhubiri bado litabaki kwa wanaume. Kulingana na kanisa, wanawake hawawezi kuwa makasisi ingawa mwaka wa 2020 Papa aliunda Tume ya kuchunguza iwapo wanawake wapewe nafasi ya kuhudumu kama makasisi.

Advertisement