Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PIC yaridhishwa na TADB

Mwenyekiti wa PIC, Jerry Silaa

Muktasari:

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imesema deni la Benki la Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) limepungua kutoka Sh300 bilioni mwaka 2020 hadi Sh67 bilioni mwaka 2021. 

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imesema deni la Benki la Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) limepungua kutoka Sh300 bilioni mwaka 2020 hadi Sh67 bilioni mwaka 2021. 

 Hayo yamesemwa leo Ijumaa Septemba 3, 2022 Mwenyekiti wa PIC, Jerry Silaa baada ya kuchambua taarifa ya utendaji wa benki hiyo.

Amesema madeni ya benki hiyo yamepungua kutoka Sh260 bilioni mwaka 2019, mwaka 2020 madeni yalikuwa ni Sh300 bilioni wakati mwaka yalikuwa ni Sh67 bilioni.

Pia amesema benki hiyo mwaka 2019 ilipata faida ya Sh3.06 bilioni, mwaka 2020 walipata faida ya Sh8.22 bilioni na mwaka 2021 walipata faida ya Sh10.9 bilioni.

Amesema kumekuwa na ongezeko la mtaji wa benki hiyo ukilinganisha na mwaka wa fedha 2020 ilipokuwa na mtaji wa Sh76.7 bilioni ambao umeongezeka kufikia Sh285.6 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 285 mwaka jana.

“Serikali ya Rais Mama Samia ilipoingia madarakani iliweka msisitizo katika kuongeza mtaji wa benki hii. Kulikuwa na mkopo kutoka Benki ya AfDB (Benki ya Maendeleo ya Afrika) wa Sh208 bilioni ambao Serikali ilifanya maamuzi ya kugeuza mkopo ule kuwa mtaji,” amesema.

Aidha, amesema Serikali imeongeza bajeti ya kilimo ambayo itatengeneza miundombinu ya kilimo na hivyo wakulima watahitaji vifaa ikiwemo natrekta kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kilimo.

Amesema ili kufanikiwa zaidi, kamati yake imeamua kukaa na Serikali kuishauri ifanye jitihada za makusudi kuongeza mtaji kwenye benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Frank Nyabundege, amesema kamati hiyo imewapa maagizo saba ya kwenda kuyatekeleza na kwamba watakwenda kujipanga kuhakikisha maagizo waliyopewa yanatekelezwa.

Amesema hadi kufikia sasa benki hiyo, imetoa mikopo kwa wakulima milioni 1.5 yenye thamani ya Sh429.5 bilioni katika mikoa 27 nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ishmael Kasekwa amesema benki hiyo imechagiza maendeleo kwa kutoa mikopo na hivyo wanaamini kutakuwa na mabadiliko kwenye kilimo kwa kukifanya kuwa cha kisasa na chenye tija.