Polisi Lindi yanasa watu 259 makosa ya uhalifu Machi

Kamanda wa polis mkoa Lindi Pili Mande. Picha Mwanja Ibadi

Lindi. Jeshi la Polisi mkoani Lindi linawashikilia watu  259 Kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kukutwa na  meno ya tembo 34 na vipande 14.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake  leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande amesema  matukio hayo ya yametokea  kipindi cha  mwezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa Lindi amesema kuwa kwa kipindi hiko  wamefanikiwa kufanya misako na dori na kuwakamata watuhumiwa 256 akiwemo wa meno ya tembo, mbao, mkaa, bangi na vifaa vya ndani ikiwemo televisioni na pikipiki.

Ofisa Mwifadhi Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Lukas Sabida amesema kumekuwa na changamoto ya uvunaji wa miti katika misitu ya hifadhi huku changamoto hiyo ikitokana na uanzishwaji wa mashamba mapya.

Amesema kwa kipindi cha miezi mitatu wakala kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo limeweza kukamata mbao 729 za ujazo wa 2'' × 8" za mti wa mkongo na mninga pamoja na mashine msumeno wa moto.