Polisi Pwani kufuatilia madai ya kukamatwa msanii Vitali

Wednesday November 03 2021
vitalispic

Msanii wa muziki, Vitali Maembe

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema linafuatilia madai ya msanii wa muziki, Vitali Maembe kukamatwa na Jeshi hilo wilayani Bagamoyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Alhamisi Novemba 3, 2021 Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Wanko Nyigesa amesema ameyasikia madai ya kukamatwa kwa msanii huyo hivyo anafuatilia ili kupata ukweli na kulitolea majibu.

Taarifa za kukamatwa Maembe ambaye alipata umaarufu kupitia wimbo wa ‘Sumu ya Teja’ zimesambaa katika mitandao ya kijamii.


Endelea kufuatikia mitandao ya kijamii ya Mwananchi kujua sakata hili.

Advertisement