Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi waendesha msako tukio la mama na mwanaye kufia gesti

Mama na mwanaye wakutwa wamekufa gesti

Muktasari:

  • Irene Lyimo(21) mkazi wa  kata ya Kilema  Kaskazini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na mwanaye wa mwaka mmoja wamekutwa wamekufa katika nyumba ya kulala wageni.

Moshi. Irene Lyimo(21) mkazi wa  kata ya Kilema  Kaskazini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na mwanaye wa mwaka mmoja wamekutwa wamekufa katika nyumba ya kulala wageni.

Akizungumza leo Jumanne Machi 2, 2021 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema mwili wa mwanamke huyo na mwanaye imekutwa jana katika nyumba moja ya kulala wageni kata ya Marangu Magharibi.

Amesema mwanamke huyo aliingia kwenye nyumba hiyo akiwa na kijana mmoja, “huyu mwanamke kuna kijana mmoja aliingia naye gesti lakini baadaye huyo kijana alitoweka hakuonekana tena mpaka huyu mwanamke alipokutwa amekufa.”

Ameibainisha kuwa wanaendelea kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumsaka kijana huyo.