Polisi waimarisha ulinzi uchaguzi Bawacha usiku

Hatimaye Askari wa Jeshi la Polisi wamewasili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, kuimarisha ulinzi.
Kuwasili kwa askari hao, kunakuja muda mfupi baada ya kushuhudiwa vurugu katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha).
Vurugu hizo zilikuwa kati ya wafuasi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wale wa Makamu Mwenyekiti wake Bara, Tundu Lissu.
Askari wa jeshi hilo, wamewasili katika eneo hilo, saa 7:00 usiku wakiwa kwenye gari kutokea Ubungo.
Baada ya polisi kuegesha gari lao, baadhi ya askari walishuka kuzunguka eneo hilo, huku wengine wakibaki ndani ya gari.
Kulikuwepo na wengine waliokwenda kwa walinzi wa mkutano huo kwa mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mmoja alikwenda ukumbini.
Pamoja na ujio wa askari hao, bado kulikuwa na vijana mbalimbali waliokaa katika vikundi nje ya ukumbi huo.
Endelea kufuatilia katika mitandao ya Mwananchi