Polisi yadaiwa kukamata viongozi Bavicha

Polisi yadaiwa kukamata viongozi Bavicha

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linadaiwa kuwashikilia viongozi watatu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) kwa madai ya kuandaa mkutano kuhusu Katiba bila kibali.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linadaiwa kuwashikilia viongozi watatu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) kwa madai ya kuandaa mkutano kuhusu Katiba bila kibali.

Hata hivyo, Mwananchi ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi kuthibitisha habari hizo hakuweza kupatikana huku simu yake ya mkononi ikipokelewa na msaidizi wake aliyesema Kamanda yupo kwenye kikao.

Awali, barua ya Polisi iliyopatikana mitandaoni na iliyosainiwa na na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Ilemela, Shamila Mkomwa ya Julai 16,2021 akiwaonya Bavicha kutofanya mkutano huo kwa kuwa haukuwa na kibali.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Julai 17, Msemaji wa Bavicha Apolnary Margwe amewataja viongozi waliokamatwa kuwa ni Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo, Richard Kaunya, Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Mwanza, Boniface Nkobe na mhamasishaji wao, Kamanda Paulina.

"Viongozi wetu wamekamatwa wakiwa wanafanya maandalizi ya mkutano ukumbini," amedai Margwe.

Mwananchi bado inafuatilia habari hizo.