Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yamshikilia Mhadhiri UDOM, wenzake wang'aka

Mwonekano wa Jengo la Utawala la Udom. Picha ya Mtandao

Muktasari:

  • Ni Melkisedeki Kaijage anayedaiwa kushikiliwa kwa madai ya kuhamasisha maandamano ya Julai 7,2026 kwa njia ya mitandao ya kijamii

Dar es Salaam. Jumuiya ya Wafanyakazi wa Kitaaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imeibua malalamiko ikidai ni ukiukwaji wa haki za msingi za mtuhumiwa, baada ya mhadhiri wa chuo hicho, Melkisedeki Kaijage, kushikiliwa na Polisi kwa siku kadhaa bila kufikishwa mahakamani.

Jumuiya hiyo imesema ina wasiwasi na mwenendo wa shauri hilo, ikieleza licha ya Kaijage kutuhumiwa kwa kosa linalodhaminika, jitihada za kumpatia dhamana hazijafanikiwa, hali iliyolazimu kufungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Leo Jumatatu, Julai 20, 2026, Mwananchi limezungumza na Katibu wa UDOMASA, Isaac Mahenge kuhusu taarifa hiyo na kudhibitisha ni taarifa rasmi waliyoitoa Julai 19, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mahenge, Kaijage alipokea wito wa kuripoti Kituo cha Polisi UDOM Julai 3, 2026 na Julai 8 alikwenda kituoni akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo pamoja na mhadhiri mwenzake.

"Baada ya Kaijage kufika kituoni, aliwekwa chini ya ulinzi kwa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO), kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baadaye kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhamasisha maandamano ya Julai 7 kupitia mitandao ya kijamii," imeeleza taarifa hiyo.

UDOMASA imesema baada ya mahojiano hayo iliomba Kaijage apewe dhamana, lakini ombi hilo halikukubaliwa licha ya kueleza kosa analotuhumiwa nalo linaruhusu dhamana.

"Kaijage baadaye alihamishiwa Kituo Kidogo cha Polisi Chang'ombe, huku uongozi wa UDOMASA ukiendelea kufuatilia suala hilo na kushirikiana na familia yake," imeeleza taarifa hiyo.

Baada ya wanataaluma wenzake hao kuona juhudi za kupata dhamana kupitia polisi hazizai matunda, UDOMASA imesema ilipeleka shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Julai 17 na kuahirishwa hadi kesho Jumanne, Julai 21, 2026.

Katika taarifa yake, UDOMASA imesema inatetea haki za wafanyakazi wake na inaamini taratibu za kisheria zinapaswa kuzingatiwa kwa mtuhumiwa yeyote bila kujali aina ya tuhuma zinazomkabili.

Tangu jana hadi leo Jumatatu, Mwananchi limeendelea kulisaka Jeshi la Polisi mkoani humo juu ya kushikiliwa kwa mhadhiri huyo na hatua wanazochukua.