Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yamwachia Kweka kwa dhamana

Muktasari:

  • Taarifa za kukamatwa kwa Kweka zilitolewa Desemba 29, 2025 na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, David Misime baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mwananchi huyo ambaye anaishi nchini Marakeni alitekwa mkoani humo.

Moshi. Jeshi la Polisi limemwachia kwa dhamana Thadey Kweka, ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania.

Raia huyo alikuwa akishikiliwa tangu Desemba 28, 2025 katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuachiwa kwake leo Januari 3, 2026.

"Ni kweli tumemwachilia kwa dhamana leo kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili," amesema Kamanda Maigwa. 

Taarifa za kukamatwa kwa Kweka zilitolewa  Desemba 29, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mwananchi huyo ambaye anaishi nchini Marakeni alitekwa mkoani humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda Maigwa imeeleza kuwa Kweka alikamatwa kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zikimkabili, mojawapo ikiwemo uchochezi.