Polisi yataja chanzo mauaji ya wapenzi
Muktasari:
- Saa chache baada ya wapenzi kukutwa wamekufa, huku mwanamke akiwa amechinjwa na mwanaume akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje, Jeshi la Polisi limeeleza chanzo cha mauaji hayo.
Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema kuwa chanzo cha mauaji ya wapenzi wawili waliokutwa wamekufa usiku wa kuamkia leo kwenye Mtaa wa Oysterbay katika Kata ya Dodoma Makulu ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Martin Otieno amesema leo Jumatatu Septemba 18, 2023 amesema tukio hilo limetokea kwa tukio usiku wa kuamkia jana na kuwataja wapenzi hao ni Samira Mathias (Esther Isugilo) na mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Amos.
Amesema mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Amos alimchoma kisu maeneo ya shingoni Samira maeneo ya shingoni kama mara tatu hivi na kupelekea koromeo kutoka nje na akawa amemchoma kwenye mkono begani.
“Lakini yeye baada ya kufanya tukio hilo akawa amejichoma kisu eneo la tumboni kwenye kitovu ambao ulipelekea utumbo wote kutoka nje na yeye mwenyewe kusababisha kifo,”amesema.