Prince Charles kurithi kiti cha ufalme
Muktasari:
- Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, Prince Charles ndiye atarithi mikoba kutokana na kifo cha mama yake.
Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, Prince Charles ndiye atarithi mikoba kutokana na kifo cha mama yake.
Prince Charles ambaye ni baba wa William na Harry, ndiye atashika kiti hicho.
Kwa sasa Prince Charles yuko kwenye makazi ya malkia Balmoral, Scotland na wanafamilia wengine waliokusanyika leo Alhamisi, Septemba 8, 2022, anatarajiwa kurejea jijini London kesho, Ijumaa Septemba 9, 2022.
Malkia Elizabeth amefariki muda mfupi uliopita wakati akiwa chini ya uangalizi maalumu ya madaktari kutokana na afya yake kutetereka.