Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malkia Elizabeth afariki dunia

Muktasari:

  • Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia muda mfupi uliopita wakati akipatiwa matibabu. Malkia huyo ambaye alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku kadhaa sasa kutokana na afya yake kutetereka.

Malkia Elizabeth wa Uingereza amefariki dunia muda mfupi uliopita wakati akipatiwa matibabu. Malkia huyo ambaye alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku kadhaa sasa kutokana na afya yake kutetereka.

Habari kutoka makazi yake huko Balmoral huko Scotland zimeeleza kuwa, afya ya malkia ilibadilika ghafla leo Alhamisi Septemba 8,2022 na kulazimika familia yake kukutana kwa dharura.

Kutokana na kifo hicho, mtoto wa Malkia Elizabeth, Prince Charles sasa ndio atakuwa mfalme na anatarajiwa kurejea jijini London kesho, Ijumaa Septemba 9, 2022.