Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Chad afariki baada ya kupambana na waasi

Rais Chad afariki baada ya kupambana na waasi

Muktasari:

  • Idriss Deby, ambaye ndio kwanza ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Chad na ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30, amefariki leo Jumanne kutokana na majeraha aliyopata wakati akipambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo, jeshi limesema leo Jumanne.

N'Djamena, Chad (AFP). Idriss Deby, ambaye ndio kwanza ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Chad na ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30, amefariki leo Jumanne kutokana na majeraha aliyopata wakati akipambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo, jeshi limesema leo Jumanne.

Deby, 68, "amevuta pumzi yake ya mwisho katika taifa hili akiwa uwanja wa vita mwishoni mwa wiki", alisema Jenerali Bermandoa Agouna katika taarifa iliyosomwa na kituo cha serikali cha televisheni.

Jumatatu, jeshi lilitangaza kuwa mapigano yalisababisha waasi 300 wa kikundi cha Front for Change and Concord in Chad (FACT) kufariki, wakati FACT ilidai katika taarifa yake kuwa Deby alijeruhiwa -- ripoti ambayo mamlaka hazikuthibitisha.

Deby, mwanajeshi ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 1990, alitangazwa kuwa ameshinda tena uchaguzi wa rais Jumatatu jioni kwa kupata asilimia 80 ya kura.

Mawaziri na maofisa wa juu wa jeshi walisema jana Jumatatu kuwa Deby alikuwa eneo hilo Jumamosi na Jumapili baada ya waasi kuanzisha mapambano kutoka kambi yao iliyo nchini Libya siku ya Aprili mosi ambayo uchaguzi ulikuwa unafanyika.

Matokeo hayakuwa na shaka yoyote kutokana na wapinzani kugawanyika, kutaka wagomee na kampeni ambazo hazikuwa na maandamano kwa kuwa yalipigwa marufuku au kutawanywa.