Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Kabila aikumbuka Tanzania kwa amani,utulivu

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania katika Ikulu ya nchi hiyo kuhusu mambo mbalimbali aliyoweza kufanya tangu alipoingia madarakani baada ya kifo cha baba yake Laurent Kabila. Picha na Boniface Meena

Muktasari:

Alisema kitu muhimu ambacho anakumbuka kuhusu Tanzania ni kwamba ni nchi yenye amani na utulivu.

RAIS wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila ameikumbuka Tanzania na kusema kuwa harakati za kuikomboa nchi yao walizifanya nchini humo kama walivyofanya baadhi ya marais wengine wa Afrika.

Rais Kabila alisema hayo jana Ikulu mjini Kinshasa wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari wa Tanzania walioko nchini Congo kwa ziara ya siku tano ya kikazi.

Alisema yeye binafsi amewahi kuishi maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Nairobi nchini Kenya, Kampala nchini Uganda na Dar es Salaam nchini Tanzania.

“Tanzania ni nchi ambayo ilitukaribisha wakati tukiwa katika harakati zetu kama ilivyofanya kwa Samora Machel, Joachim Chissano na wengine,”alisema Rais Kabila.

Hata hivyo pamoja na kueleza hayo Rais Kabila hakutaka kuelezea kama Serikali ya Tanzania iliwasaidia vipi kuhakikisha wanaikomboa nchi ya Congo kutoka kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mobutu Seseko.

“Kuhusu  kama  tulisaidiwaje hilo ni jambo ambalo siwezi kulizungumzia hapa, nikija Dar es Salaam ninaweza kuwaeleza na hata kuwaonyesha niliishi maeneo  gani katika jiji la Dar es Salaam,”alisema Rais Kabila.

Alisema kitu muhimu ambacho anakumbuka kuhusu Tanzania ni kwamba ni nchi yenye amani na utulivu.

Akizungumzia mikakati mbalimbali ya Serikali yake na changamoto katika kuijenga nchi ya Congo,  Rais Kabila alisema hivi sasa wameweza kuibadilisha nchi hiyo na kuwa nchi inayoweza kukalika kwa amani isipokuwa eneo moja tu la Mashariki ambalo limekuwa na vita kila wakati.

“Suala la vita Mashariki ni matatizo ambayo tumeyarithi na kwamba yako kuanzia miaka ya 60 lakini vile vita vingine tulivyokuwa navyo nchini viliisha mwaka 2009 , hivi sasa tunajitahidi kuleta amani Mashariki ya Congo,”alisema Rais Kabila.

Alisema ukosefu wa amani katika eneo hilo unasababishwa na nchi jirani hasa Rwanda hivyo wanajitahidi kuhakikisha hilo lina kwisha kwa njia ya mazungumzo.

“Hivi sasa lengo letu kubwa ni kufikia amani ya kudumu kwa kuzungumza. Sasa muda umefika kwani tunachotaka ni amani,”alisema Rais Kabila.

Alisema amekutana na viongozi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), ili kuweza kuhakikisha amani katika eneo la Mashariki ya Congo inapatikana kwa mazungumzo na si vinginevyo.

“Inanishangaza sana kwa nini watu wanafanya vita eneo la Mashariki mwa Congo wakati ndilo eneo kubwa la biashara kwa nchi wanaozunguka eneo hilo,”alisema na kuongeza:

“Sisi nia yetu ni kuhakikisha tunakuwa na uhusiano mzuri na hata muda ukifika tutafanya mazungumzo ili tuweze kuwa na wawakilishi wetu kwenye EAC.”

Akizungumzia maendeleo ya nchi yake alisema wamejitahidi katika kujenga miundombinu ya nchi ili kurahisisha ufanywaji wa biashara na kuiboresha nchi ya Congo na kukuza uchumi wa nchi ambao unakua taratibu bila kueleza hivi sasa uchumi wao ni asilimia ngapi.

Mbali na hilo Rais Kabila alisema katika sekta ya madini wameanza mchakato wa kitengeneza sheria mpya ya madini ili Serikali iweze kufaidika zaidi na rasilimali hiyo.

“Sekta ya madini tangu tulipopata uhuru ilikuwa chini ya mikono ya Serikali hivi sasa tunakusanya fedha ili tuweze kufanya uzalishaji wenyewe na si kutegemea wawekezaji,”alisema Rais Kabila.

Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa kumekuwa na matatizo hasa kwenye miradi ya wafadhili kuchelewa kukamilika hasa kwenye suala la upembuzi yakinifu kufanyika muda mrefu kusikokuwa na faida.

Alisema hivi sasa mambo matatu yanayomnyima usingizi ni kukosekana kwa amani katika baadi ya maeneo ya Congo, uimara wa siasa za Congo na hali ya uchumi.

“Ukiniuliza kitu ambacho kinaniumiza kichwa na kunifanya nikose usingizi ni amani na ndiyo suala kubwa zaidi, uchumi pia kwani kwa asilimia kubwa wakazi wa mijini ni vijana na wanahitaji ajira pamoja na suala la political stability (utulivu wa kisiasa),”alisema na kuongeza kuwa:

“Nahitaji haya mambo yawe sawa ili nisiwe na mawazo makubwa sana, nikifanikiwa haya mambo yatakuwa mazuri.”