Rais Samia aridhia ombi la kuwamilikisha maofisa ugani pikipiki

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  •  Rais Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la Waziri Kilimo, Hussein Bashe la kuwamilikisha maofisa ugani pikipiki walizopatiwa leo baada ya miaka miwili ziwe mali yao kwa masharti ya kupimwa kwa kuhuduma watakazotoa.


Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la Waziri Kilimo, Hussein Bashe la kuwamilikisha maofisa ugani pikipiki walizopatiwa leo baada ya miaka miwili ziwe mali yao kwa masharti ya kupimwa kwa kuhuduma watakazotoa.

Aidha, Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila kuwashughulikia kisawasawa waliobainika kuiba fedha za ushirika na pembejeo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 4,2022 wakati akizindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.

“Tukiwaambia watazitunza na wakijua miaka miwili tunawapa watazitunza na kwa muda huo dhamani ya huduma itakuwa imetimia. Tutawapima kwa huduma, tutapima kwa kazi mnazofanya. Nimelikubali hili (ombi la kuwaachia pikipiki kwa miaka miwili lakini litakwenda na masharti yake,”amesema.

Kuhusu walioiba fedha za umma mkoani Simiyu, Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa huo David Kafulila kuwashughulikia sawa sawa wezi hao.

Amesema wengine wenye nia ya kuziiba wakishazisoma rangi za viongozi kwa watakavyoshughulikiwa watuhumiwa hao hawataiba.

“Nataka uwashughulikie kisawasawa. Nimeambiwa umewakamata wa ruzuku na walioiba fedha za ushirika. Nataka uwashughulikie kisawasawa na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) ulisimamie hili,”amesema.