Rais Samia ateua majaji 22

Rais Samia ateua majaji 22

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua maofisa 22 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo Jumamosi, Agosti 6, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imesema mkuu huyo wa nchi alifanya uteuzi huo juzi Alhamisi Agosti 4, 2022.

Miongoni mwa walioteuliwa kuwa majaji wa Mahakama Kuu ni pamoja na Gabriel Pascal Malata ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Kevin Mhina.


Majaji hao walioteuliwa ambao tarehe ya kuapishwa itatangazwa ni;


1. Kevin David Mhina- kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani

2. Gabriel Pascal Malata-kabla ya uteuzi huu alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali

3. Adrian Philbert Kilimi- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili Mahakama

4. Happiness Philemon Ndesamburo- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama;

5. Victoria Mlonganile Nongwa- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

6. Obadia Festo Bwegoge- kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

7. Ruth Betwel Massam-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

8. Godfrey Ntemi Isaya-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

9. Gladys Nancy Barthy-kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama

10. Haji Suleiman Haji- kabla ya uteuzi alikuwa Mwendesha Mashitaka Mfawidhi Mahakama Kuu, Zanzibar

11. Fatma Rashid Khalfan-kabla ya uteuzi alikuwa Kamishna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

 12. Abubakar A. Mrisha-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Serikali

13. Lusungu Hemed Hongoli-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

14. Monica Peter Otaru-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

 15. Kamana Stanley Kamana-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi Msaidizi (Tamisemi)

 16. Hamidu Rajabu Mwanga-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi

17. Marlin Leonce Komba-kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

18. Dk Mwajuma Kadilu Juma-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Mzumbe

19. Dk Cleophas K.K. Morris-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu Dar es Salaam

20. Asina A. Omani-kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

21. Aisha Zumo Bade- kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea

22. Mussa Kassim Pomo-kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Taarifa hiyo imesema kuwa tarehe ya kuapishwa majaji hao wateule itatangazwa baaadaaye.