Rais Samia awaita Mwigulu, Kijaji na bosi TRA Ikulu

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amefanya kikao maalum na watendaji mbalimbali wa wizara ya fedha na mipango wakiongozwa na Waziri wake, Dk Mwigulu Nchemba, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakiongozwa na Waziri wake, Dk Ashatu Kijaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna Mkuu Alphayo Kidata pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka. Kikao hicho kimefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao baina yake na vigogo wa wizara wa Fedha na Mipango, Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mawaziri, Dk Mwigulu Nchemba wa fedha na mipango, Dk Ashatu Kijaji wa viwanda, biashara na uwekezaji, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata pamoja na watendaji wao wameshiriki kikao hicho. Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka.

Kikao hicho kimefanyika leo Alhamisi, Mei 17 Ikulu ya Dar es Salaaam ikiwa ni siku moja kupita tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuumaliza mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo uliokuwa umedumu kwa siku tatu kuanzia Jumatatu ya Mei 15 hadi 17, 2023.

Katika kikao hicho, mawaziri wa fedha, Dk Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Ashatu Kijaji, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kijaji waliokuwapo walishtumiwa kwa na wafanyabiashara hao kushindwa kuwawekea mazingira mazuri ya biashara.

Vitendo vya rushwa, manyanyaso kutoka kwa watumishi wa TRA, Jeshi la Polisi pamoja na kodi ya stoo vilikuwa miongoni mwa shtuma zilizotolewa huku Waziri Mkuu akivitaka vyombo, TRA na Jeshi la Polisi kujitafakari kutokana na kile kilichoelezwa na wafanyabiashara.

Mbali na Dk Mwigulu, Dk Kijaji, wengine waliokuwapo kwenye kikao hicho cha Majaliwa kilichofanyikiwa Viwanja vya Mnazi Mmoja ni mawaziri, Angellah Kairuki wa Tamisemi, Hamad Masauni wa Mambo ya Ndani pamoja na Katibu Mkuu-Ikulu, Mululi Majula Mahendeka.

Majaliwa aliunda kamati ya watu 14 ukijumuisha maofisa wa Serikali na wale miongoni mwa wafanyabiashara kwenda kupitia changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kuona jinsi ya kuishughulikia.