Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia kuongoza waombolezaji kumuaga Membe

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

  •  Rais Samia kuongoza waombolezaji kumuaga aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne Benard Membe

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, leo Mei 14, 2023 anatarajiwa kuwaongeza mamia ya waombelezaji waliofika katika viwanja kwa Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe.

Membe alifariki asubuhi ya Mei 12, 2023 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.

Ratiba ya kumuaga Membe ilianza asubuhi ya leo nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako ilifanyika ibada takatifu kabla ya shughuli ya kitaifa kufanyika katika viwanja vya Karimjee.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wamewasili katika hafla hiyo akiwemo Naibu Spika Mussa Zungu, Waziri wa Mambo ya Nje, Stargomena Tax na Kamishna wa Uhamiaji, Anna Makakala.

Wapo pia mawaziri na wabunge wa zamani waliowahi kufanya kazi na Membe akiwemo Lazaro Nyalandu, Fenela Mukangara, Stephen Wasira, William Ngeleja na Godbless Lema ambaye ni kiongozi wa Chadema.

Baada ya shughuli ya kutoa heshima za mwisho kukamilika jijini hapa mwili wa Membe utasafirishwa kesho Mei 15, 2023 kuelekea katika kijiji cha Chiponda kata ya Rondo mkoani Lindi ambako maziko yatafanyika Mei 16 mwaka huu.