Rais Samia ziarani siku tatu Kagera

Muktasari:
- Rais Samia Suruhu Hassan anatarajia kuwa na ziara ya siku tatu mkoani Kagera kuanzia June 08, hadi June 10, 2022.
Bukoba. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa na ziara ya siku tatu mkoani Kagera ambapo katika ziara hiyo ataziandua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh15 bilioni pamoja na kuzindua msikiti wa Istiqama.
Taarifa ya ujio wa Rais Samia Suruhu Hassan imetolewa leo Juni 05, 2022 na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Generali Charles Mbuge wakati akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vilivyopo mkoani Kagera.
"Rais wa nchi hii Samia Suluhu Hassan anatarajia kuingia mkoani hapa Juni 08, 2022 kupitia barabara ambapo tutampokea maeneo ya Bwanga wilaya ya Biharamlo atasalimiana na wananchi katika eneo hilo na maeneo yenye mkusanyiko wa watu atakapopita katika wilaya za Biharamlo, Muleba, Bukoba vijijini na Bukoba mjini Amesema Meja Generali Mbuge
Ameongeza kwamba, Juni 09, 2022 atazindua mradi wa maji wa Kyaka- Bunazi katika wilaya ya Missenyi wenye thamani ya zaidi ya Sh15.7 bilioni na atatembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kiwanda cha Kagera Sukari.
Vile vile Juni 10,2022 ataongea na watanzania kupitia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa michezo Kaitaba ulipo Bukoba na baada ya hapo atazindua msikiti wa Istiqama uliopo Manispaa ya Bukoba uliojengwa kwa ufadhili wa Istiqama Tanzania.
Aidha Mbunge ameitaka jamii mkoani Kagera kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Rais katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Bukoba mjini na maeneo mengine atakapokuwa anapita akisalimiana na wananchi.