Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Katavi atoa onyo ucheleweshaji ujenzi bwawa la maji Mlele

Bwawa la maji Senkwa lililopo wilayani Mlele ambalo lilianza kujengwa Agosti 2018 na lilitakiwa kukamilika Septemba 2019 lakini hadi sasa halijakamilika. Picha na Mary Clemence

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ametoa onyo kwa mkandarasi Hematake Investment kuacha kutoa visingizio visivyokuwa na msingi vya kuchelewesha mradi wa bwawa la maji Senkwa wilayani Mlele.

Katavi. Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ametoa onyo kwa mkandarasi Hematake Investment kuacha kutoa visingizio visivyokuwa na msingi vya kuchelewesha mradi wa bwawa la maji Senkwa wilayani Mlele.

Mwanamvua ametoa onyo hilo leo Jumapili Augosti 28, 2022 baada ya kukagua mradi huo na kubaini uzembe uliosababisha mradi huo kutokamilika ndani ya miaka mitano ambapo ni nje ya mkataba.

“Mkandarasi una matatizo kasi ni ndogo sana, unasingizia masika ulishindwa kufanya kazi je kiangazi umefanya nini? unaniambia ulikuwa unarekebisha magari hili siyo suala la serikali,

“Tatizo lingine lipo kwa Ruwasa makao makuu wenyewe tumeambiwa barua zinaandikwa, mawasiliano yanafanyika kuanzia 2018 hadi 2022 lakini ufumbuzi hakuna,” amesema Mrindoko.

Kutokana na hali hiyo ametoa rai kwa Waziri wa Maji na RUWASA makao makuu kufika eneo hilo kubaini tatizo linalosababisha mradi uchelewe na watafutie ufumbuzi.

“Hatuwezi kuendelea namna hii tutajikuta unatekelezwa miaka saba, wananchi vijiji 16 wanasubiri maji,   wizara wana ufumbuzi wake na RUWASA wilaya simamieni changamoto zilizopo,”

Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya Hematake Investment, Lendnand Mawe amesema mradi huo ulitakiwa kukamilika 2019 na changamoto zilizosababisha usikamilike ni upatikanaji wa mawe ulikuwa mgumu.

“Tunafuata kilometa sita kutoka eneo la mradi, kipindi cha mvua ni changamoto tunatumia miezi mitano tu kwa mwaka kufanya kazi,”amesema

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mlele, Gilbart Izack amesema mradi huo upo hatua za ukamilishaji na bwawa hilo lina uwezo wa kuvuna lita bilioni mbili kwa mwaka.

“Mradi huu ukikamilika utahudumia vijiji 16 na unagharimu Sh1.8 bilioni, ulianza kutekelezwa Agosti 3, 2018 ulitakiwa kukamilika Septemba 30, 2019,”

Amesema kilichochangia mradi huo kushindwa kukamilika kwa wakati ni kutokana na kujengwa kwa udongo hivyo wakati wa masika mkandarasi hafanyi kazi.