Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Sendiga atangaza vita Iringa

RC Sendiga atangaza vita Iringa

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema mwananchi atakayekamatwa na mafuta yanayotumika katika  mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuhujumu miundombinu ya Serikali.

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema mwananchi atakayekamatwa na mafuta yanayotumika katika  mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Nduli atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuhujumu miundombinu ya Serikali.

 Sendiga amesema hayo wakati akikagua mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Sino Hydro ya nchini China  baada ya kupokea taarifa kutoka polisi kwamba kuna watu wamekamatwa wakiw ana gari lililopakia madumu ya mafuta yaliyoibwa katika eneo la mradi.

Amesema hatokuwa tayari kuona fedha za Serikali zikipotea bure wakati Serikali imewekeza Sh41 bilioni za upanuzi wa kiwanja hicho.

"Yeyote atakayehusika na wizi wa mafuta kesi ya uhujumu uchumi itamuelemea sio muda mrefu, nitakayempata hata ana kidumu kimoja nyumbani kwake au kakamatwa nayo popote pale kesi ya uhujumu uchumi itamuhusu sioni sababu ya vijana kuiba vifaa na mafuta kwa sababu hawajapata ajira katika mradi huu kwa sababu wengi hamkukidhi vigezo.”

"Waliokamatwa leo nataka wafikishwe mahakamani haraka sana kwa sababu wamekamatwa na kidhibiti hivyo sitarajii kuona upelelezi unachukua muda mrefu wakati watuhumiwa wamekamatwa na kielelezo"amesema