RC Shinyanga awataka wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amewataka wafanyabiashara wote wa mkoa huo kulipa kodi kwa wakati ili kukamilisha mwaka wa fedha 2021/2022.


Shinyanga. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amewataka wafanyabiashara wote wa mkoa huo kulipa kodi kwa wakati ili kukamilisha mwaka wa fedha 2021/2022.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema baadhi ya wafanyabiashara hawajalipa kodi hadi sasa na wengine wanadaiwa madeni ya muda mrefu.

Amewataka wafanyabiashara hao kulipa kodi kabla ya June 20, 2022.

"Nawaombeni sana wananchi wote ambao bado mnadaiwa kodi mlipe kwa wakati pia muwasilishe ritani ya VAT na mlipe kabla ya juni 20 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya zuio SDL na PAYE kabla ya tarehe 7 juni mwaka huu "amesema Mjema.

Pia Mjema amewaomba wananchi wote siku ya Agosti 23 waweze kujitokeza katika sensa ya makazi, ili Serikali isihangaike katika kupanga bajeti za kuwahudumia wananchi kama vile madawati zahanati na huduma zingine mbalimbali.

 Kwa upande wake Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi, Edwin Iwato amesema wameanzisha kampeni ya amsha amsha ya elimu kwa mlipa kodi mlango kwa mlango, ili kuwakumbusha wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati.

"Dira ya mapato ni kuongeza makusanyo ya ndani, kinachotakiwa walipe kodi kwa hiari kwani kufanya hivyo ni kujiletea maendeleo wenyewe na dhamira ya kampeni hii  kufanya ulipaji wa kodi kuwa mwepesi"amesema Iwato.