RC Tanga aagiza Polisi kuharakisha uchunguzi kifo cha mhandisi mradi wa EACOP

Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RC), Adam Malima

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RC), Adam Malima ameviagiza vyombo vya dola mkoni humo kuharakisha uchunguzi wa kifo cha raia wa kigeni mbaye alikuwa mhandisi mshauri katika mradi wa mradi wa Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Uganda-Tanga, Abraham Jacobus (47).

Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RC), Adam Malima ameviagiza vyombo vya dola mkoni humo kuharakisha uchunguzi wa kifo cha raia wa kigeni mbaye alikuwa mhandisi mshauri katika mradi wa mradi wa Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Uganda-Tanga, Abraham Jacobus (47).

Raia huyo wa Afrika Kusini alikuwa amefariki dunia chumbani katika moja ya hoteli maarufu jijini Tanga Mei 21 mwaka.

Malima amesema kuharakisha uchunguzi kutasaidia kuondoa sintofahamu kwa wananchi na mitandao ya jamii.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo leo Jumanne Mei 24, 2022wakati wa kikao chake na wafanyabiashara na wadau kilichoketi leo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Amesema Mkoa wa Tanga upo salama hivyo wananchi wawe watulivu kwa sasa na kwamba uchunguzi wa kifo cha raia huyo wa Afrika Kusini utafanyika ili kubaini kiini cha kifo chake.

Malima amekemea vitendo vilivyofanywa na baadhi ya watu ambao wamesambaza video na picha za marehemu katika mitandao ya kijamii amesema kiendo hicho ni kinyume na utaratibu na kwamba si cha kibinadamu.

"Kwa sasa mwili umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Bombo tuna vyombo vya dola na matabibu hivyo nuchunguzi uharakishwe ili mwili uweze kusafirishwa kwenda kwao’ amesema Malima.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David Chidingi amesema kwamba wamepokea maelekezo na kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika katika eneo la tukio  utakapokamilika taarifa zitatolewa.