Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ripoti LHRC yaonyesha ubakaji wa watoto washika kasi Tanzania

Mtafiti Fundikira Wazambi akizungumzia ripoti ya haki za binadamu kwa kipindi cha Januari mpaka June mwaka huu

Muktasari:

  • Ripoti ya haki za binadamu kuanzia Januari hadi Juni 2019 inaonyesha ubakaji wa watoto kuzidi kushika kasi nchini Tanzania

Dar es Salaam. Ripoti ya haki za binadamu kuanzia Januari hadi Juni 2019 inaonyesha ubakaji wa watoto kuzidi kushika kasi nchini Tanzania.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo Jumanne Agosti 20, 2019 na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inaonyesha Tanzania Bara  asilimia 66 ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto ni ubakaji wakati ukatili wa kimwili ukiwa asilimia 34.

Akisoma ripoti hiyo mkurugenzi wa LHRC,  Anna Henga amesema wafanyaji wakuu wa ukatili huo ni watu wa karibu wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa, majirani na walimu.

Amesema asilimia 38 ya matukio ya ukatili kwa watoto yameripotiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huku Kanda ya Nyanda za Juu Kusini hasa Mbeya, Njombe na Iringa ikiwa ni asilimia 32.

"Upande wa Mwanza ulawiti wa watoto unaofanywa na watoto wenzao umeonekana kuwa changamoto katika kata 17 ikiwemo Igofo, Igoma na Nyegezi," amesema Henga.

Mtafiti wa LHRC, Fundikira Wazambi amesema suluhisho la ukatili huo ni kwa jamii kuongeza ulinzi kwa watoto bila kumwamini yeyote.

"Usiseme muda mwingi unatafuta fedha wakati mtoto wako wanaangamia, kama baba anaweza kumbaka mwanae vipi kuhusu jirani? juhudi za kulinda watoto ziongezeke," amesema.