RPC Manyara atoa onyo wafugaji, wakulima watakaovunja sheria

Muktasari:

  • Akusudia kutatua mgogoro wa ardhi wa wakulima na wafugaji eneo la Pori namba mbili

Kiteto. Kufuatia kukithiri migogoro ya ardhi ya wakulima na wafugaji Kiteto, inayofanya makundi hayo kuhasimiana, Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara RPC George Katabazi amekusudia kukutana na makundi hayo.

RPC Katabazi ameyasema hayo jana mjini Kibaya wakati akizungumza na maofisa na wakaguzi wa Polisi Kiteto kabla ya kuanza ziara yake ya siku moja wilayani hapo.

Amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao, wakulima na wafugaji hao pamoja na mali zao wanapaswa kuwa salama na lazima walindwe alisema RPC Katabazi.

"Nitaenda kutakutana na wananchi makundi hayo na wananchi wa eneo la Pori Namba Moja na tunakusudia kuweka kituo cha Polisi kufuatia kukithiri kwa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji," amesema.

Alisema Jeshi la Polisi tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuheshimu sheria na mipango yao waliyojiwekea.

"Atakayekiuka sheria na taratibu za nchi hii Jeshi la Polisi tutahakikisha kuwa anakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.