Rushwa yawaponza watumishi wa Tanesco

Muktasari:

Walikuwa wakimtuhumu mteja kuchezea mita kwa muda mrefu na kulisababishia hasara shirika hilo

Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewaburuza kortini, watumishi wanne wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh300,000 kutoka kwa Ludovock Njau.

Watumishi hao wa Tanesco walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Moshi, Anthony Ngowi na kusomewa makosa yanayowakabili.

Waliopandishwa kortini ni Nixon Kivelege(43) msoma mita, Beth Mmbo (47), Damian Eugen (26) na Huruma Matee (30) ambao ni mafundi wa shirika hilo.

Habari zaidi soma Gazeti Mwananchi