Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saa 10 bila maji Dar, Pwani

Muktasari:

  • Dawasa yatangaza maboresho yatakayoikumba Dar, Pwani siku ya Mei 10,2026 hali itakayoababisha maeneo ya  mikoa hiyo kukosa huduma ya maji.

Dar es Salaam. Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kukumbwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa wastani wa saa 10 kesho Jumapili, Mei 10, 2026, kufuatia matengenezo kinga ya miundombinu ya umeme.

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) huduma hiyo itaathirika kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwa wananchi wanaohudumiwa kupitia mitambo ya Ruvu Chini wilayani Bagamoyo na Ruvu Juu wilayani Kibaha.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuruhusu matengenezo ya miundombinu ya umeme katika kituo cha kupooza umeme Mlandizi, hatua inayotarajiwa kusaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa muda mrefu.

Maeneo yatakayoathirika kupitia mtambo wa Ruvu Chini ni pamoja na Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbezi Beach, Kawe, Lugalo, Makongo, maeneo ya vyuo vikuu vya UDSM na Ardhi, Mwenge, Mikocheni, Masaki, Oysterbay, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni na Kigogo.

Mengine ni Chang’ombe, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na katikati ya jiji.

Kwa upande wa mtambo wa Ruvu Juu, maeneo yatakayokosa huduma ni pamoja na Ruvu Darajani, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Mbezi, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Ubungo, Ukonga, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.

Kufuatia hali hiyo Dawasa imewataka wananchi kuhifadhi maji ya kutosha kwa matumizi muhimu katika kipindi hicho cha maboresho ili kupunguza athari za ukosefu wa huduma.