Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu Malisa kupelekwa hospitali baada ya kuachiwa kwa dhamana

Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa katika hospitali ya KCMC.

Muktasari:

  • Baada ya Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa kukaa mahabusu kwa zaidi ya saa 24, katika kituo cha polisi Moshi kati, Mkoani Kilimanjaro, Mwanasheria wake, Hekima Mwasipu amesema mteja wake huyo aliugua gafla na baada ya kupewa dhamana usiku wa kuamkia leo Juni 8 alipelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu.

Moshi. Baada ya Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa kukaa mahabusu kwa zaidi ya saa 24, katika kituo cha polisi Moshi kati, Mkoani Kilimanjaro, Mwanasheria wake, Hekima Mwasipu amesema mteja wake huyo aliugua akiwa mahabusu na baada ya kupewa dhamana usiku wa kuamkia  leo Juni 8 alipelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu.

Mwasipu amesema mteja wake huyo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa, kifua, kizunguzungu na tumbo na kwamba afya yake kwa sasa imeimarika.

Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na Meya wa zamani wa ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Baada ya kukamatwa Malisa, alisafirishwa kwenda Moshi na alipofika alianza kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza na Mwananchi digital leo asubuhi, Juni 8, Mwanasheria wake, Hekima Mwasipu amesema, Malisa baada ya kukaa kituo cha polisi kati Moshi, Malisa aliugua gafla na alipopata dhamana aliwahishwa KCMC kwa matibabu.

"Tulipopata dhamana usiku wa saa 6 kituo cha polisi Moshi kati, tulimpeleka hospitali ya KCMC moja kwa moja kwa sababu alikuwa akilalamika maumivu ya kichwa, kifua, kizunguzungu na tumbo,"

"Alipatiwa matibabu na tulirudi saa 10 alfajiri, kwasasa anaendelea vizuri,"amesema wakili wake Mwasipu

Mwasipu amesema kwasasa Malisa anaendelea vizuri na leo  saa 3:00 atapaswa kuripoti kituo cha polisi Moshi kati.


 Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi