Sabaya mahakamani tena akiwa peke yake

Aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusikiliza kesi namba mbiliĀ  ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022, inayomkabili.

Muktasari:

Sabaya anakabiliwa kesi namba mbili ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022, huku wenzake alioshitakiwa nao wakiwa wameachiliwa huru baada ya kukiri kosa na kuachiliwa huru Septemba 6 mwaka huu.

Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Jumatatu Septemba 26 amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi akiwa peke yake.

Sabaya anakabiliwa kesi namba mbili ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022, huku wenzake alioshitakiwa nao wakiwa wameachiliwa huru baada ya kukiri kosa na kuachiliwa huru Septemba 6 mwaka huu.

Washirika hao ni pamoja na Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey aliokuwa.

Makosa waliyokiri ni pamoja na kujitwalia madaraka isivyo halali na kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Alex Swai na kula njama, kumnyima na kukandamiza haki yake.

Mahakama hiyo iliwatia hatiani na kutoa amri ya kulipa kila mmoja faini ya Sh50,000 na fidia ya Sh1milioni kwa mlalamikaji Alex Swai.