Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya miaka 28 iliyojaa ubunifu, ukuaji wa kasi

Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania, moja ya taasisi kinara za kifedha nchini, imeadhimisha leo miaka 28 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Miaka 28 ya Kusonga Mbele Pamoja na Wewe.”

Sherehe hizo zilizofanyika katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, ziliwaleta pamoja wafanyakazi na menejimenti wa benki hiyo, wakiwa na lengo la kutafakari safari ya Exim tangu ilipoanza mwaka 1997 hadi sasa. Safari hiyo imejaa ubunifu, ukuaji wa kasi na huduma zinazomtanguliza mteja katika kila hatua.

Kwa mujibu wa benki, mafanikio hayo yametokana na mabadiliko makubwa ya Exim kutoka tawi moja tu Mtaa wa Samora, Dar es Salaam, hadi taasisi ya kimataifa yenye matawi katika nchi za Comoro, Djibouti na Uganda. Benki hii imejikita kwenye misingi ya Uwezo wa Kubadilika, Uhakika, Uadilifu, Utaalamu na Bidii ya Kutosheleza Mahitaji ya Wateja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu, aMEsema kaulimbiu ya mwaka huu inalenga wafanyakazi na wateja wa benki. “‘Wewe’ ni kumbukumbu ya wafanyakazi wetu mahiri, ambao ndio moyo na roho ya benki hii, na pia ni wateja wetu, wanaotuamini na ndoto zao, fedha zao na maisha yao ya baadaye. Tunaposherehekea miaka 28, hatuangalii tu tulichojenga nyuma yetu, bali tunaangalia mbele, kwa yale ambayo bado tunaweza kuyafanikisha pamoja,” amesema.

Miaka ya hivi karibuni, Benki ya Exim Tanzania imepiga hatua kubwa kimasoko na kiteknolojia. Benki hiyo imeboresha mfumo wake wa msingi wa kibenki, hatua iliyowezesha kutoa huduma bunifu na kuongeza uwepo wake nchini. Hivi karibuni, benki pia ilizindua huduma mpya ikiwemo Lipa Chapchap kwa wafanyabiashara na Elite Banking kwa wateja wa kifahari, hatua zinazoiweka Exim Tanzania kileleni mwa ubunifu wa huduma za kifedha nchini.

Aidha, benki imezindua kampeni ya ‘Kopa KiBoss na Wafanyakazi Loan’, inayowezesha watumishi wa umma kupata mikopo hadi Sh. milioni 200 kwa marejesho ya hadi miaka 11 – ya kwanza kuanzishwa katika taasisi za kifedha nchini.

 Matundu alisisitiza umuhimu wa fikra za kimaendeleo katika sekta ya fedha inayobadilika kwa kasi. “Kwa mifumo na ubunifu tulioanzisha, matarajio ya wateja wetu yapo juu zaidi kuliko ilivyowahi kuwa. Ni jukumu letu kutambua mahitaji yao mapema na kuendelea kujifunza, kukua na kujiboresha ili kwa pamoja tuijenge benki na mustakabali wa kifedha tunaoweza kujivunia,” amesema.

Benki ya Exim inavyoendelea na safari yake, malengo yake ni dhahiri: kuendelea kukua, kupanua wigo wake, kuleta ubunifu na kuboresha huduma kwa wateja, sambamba na kuchangia maendeleo ya sekta ya fedha na taifa kwa ujumla.

Maadhimisho ya miaka 28 ya Benki ya Exim Tanzania ni ushahidi wa mafanikio yake, na zaidi ya yote, ni uthibitisho wa kujitolea kwake kwa mustakabali bora wa kifedha kwa Watanzania na ukanda mzima.