Samia azungumzia magonjwa yasiyoambukiza na kukua kwa teknolojia

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa sababu yanabainika kwa utahisi kutokana na kukua wa teknolojia.

T:

S:



Aurea Simtowe, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa sababu yanabainika kwa utahisi kutokana na kukua wa teknolojia.

Ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 12, 2021 katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Cathlab uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 (3D & Mappingi Electrophysiology system) uliogharimu Sh4.6 bilioni huku kazi yake ikiwa ni kuchunguza na kutibu mfumo wa umeme wa moyo.

Amesema zamani wakati hakuna utaalamu wa kuyabaini magonjwa haya watu walikuwa wanakufa bila kujua wamekufa kwa sababu gani.

“Lakini kwa sababu tumepiga hatua kwenye utaalamu sasa magonjwa haya tunayatambua na tunayajua, hivyo inawezekana yamezidi kwa sababu ugunduzi umezidi na tunayatambua,” amesema Samia.

Amesema Tanzania magonjwa yasiyoambukiza yalichangia asilimia 33 ya vifo vyote nchini kwa mwaka 2017 ambapo vifo vya magonjwa ya moyo na shinikizo la damu ni asilimia 13.

“Hii ni asilimia kubwa sana kuiacha itokee ndani ya nchi, ndiyo maana leo tuna faraja kuzindua mitambo hii ya kisasa ya uchunguzi na tiba ya magonjwa wa moyo lengo ni kupunguza hii asilimia 13 iende chini zaidi,” amesema Samia

Amesema mtambo huo ni wa kisasa tofauti na ule uliokuwepo awali kutokana na kazi inayofanya.