Samia mgeni rasmi mkutano wa Arinsa

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Austin Maiga akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Mkutano wa Umoja wa Taasisi zinazokabiriana na uharifu unaovuka mipaka utaokaofanyika kuanzia kesho. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga. Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Tanzania ni mwenyeji wa mkutano wa umoja wa taasisi zinazokabiliana na uhalifu unaovuka mipaka (Arinsa) utakaofanyika kesho Jumatano Juni 12, 2019 jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan


Dar es Salaam. Tanzania ni mwenyeji wa mkutano wa umoja wa taasisi zinazokabiliana na uhalifu unaovuka mipaka (Arinsa) utakaofanyika kesho Jumatano Juni 12, 2019 jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza kuhusu mkutano huo leo Jumanne Juni 11, 2019 waziri Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga amesema mkutano huo utaongozwa na Rais wa Arinsa, Biswalo Mganga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

"Lengo la mkutano huu ni kuhakikisha wahalifu hawanufaiki na mali za uhalifu na pia hawana mahali pa kujificha katika nchi wanachama," amesema Dk Mahiga.

Waziri huyo amebainisha uhalifu wanaoshughulika nao ni utakatishaji wa fedha, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya usafirishaji binadamu, uhalifu wa mtandao na ugaidi.