Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samia: Msihujumu miradi ya wawekezaji

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

  • Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Mara ambako alikagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha chaki na kutembelea eneo litakalojengwa kiwanda cha sukari.

Tarime. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi waache tabia ya kuhujumu miradi ya  wawekezaji kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Mara ambako alikagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha chaki na kutembelea eneo litakalojengwa kiwanda cha sukari.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tabia ya wananchi kupinga kila kitu hata uwekezaji haifai hata kidogo kwani inachangia kuzorotesha shughuli za maendeleo hivyo ni lazima ikomeshwe.

“Shirikianeni  na wawekezaji wanaokuja nchini kwani kufanya hivyo taifa litapata mapato na wananchi watapata ajira kwenye viwanda vitakavyojengwa nchini,” amesema

Akihutubia wananchi wa kijiji cha Biswari katika mkutano wa hadhara, Mama Suluhu ameunga mkono kauli ya wananchi wa Tarime ya kutaka kuharakishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika Bonde la Mto na kusema uwekezaji huo utaongeza maradufu mapato ya halmashauri ya Tarime na kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa mkoa huo.

Amesema ataiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuharakisha mchakato wa kutoa vibali ili shughuli za kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda hicho cha miwa kujengwa haraka na kuanza kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Wawekezaji hao kutoka nchini Uganda wanataka kujenga kiwanda sukari na kuanzisha kilimo cha miwa kwenye eneo la ekari zaidi ya elfu 30 katika bonde la Mto wilayani Tarime.

Kuhusu kilimo cha bangi wilayani Tarime, Mama Suluhu amewaagiza wote wakaze kamba katika kupambana na kilimo hicho ili kikomeshwe wilayani huo.

“Viongozi katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla washirikiane katika kukomesha kilimo hiki ambacho kimekithiri wilayani Tarime,” amesema

Kuhusu Kero ya maji wilayani Tarime, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua tatizo hilo na itafanya kila inavyowezekana ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wa wilaya ya Tarime.

Amesema Serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha tatizo la maji linakuwa historia nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za kiuchumi ipasavyo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali ya mkoa huo imejipanga vyema ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii kwa wakati pamoja na kuimarisha hali ya ulinzi usalama kwa wananchi mkoani humo.