Samia: Rais mwanamke tutamuweka 2025

Wednesday September 15 2021
samiapiccc

Rais Samia Suluhu Hassan

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan amesema wanawake watamuweka madarakani rais mwanamke mwaka 2025.

Samia aliapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli. Kabla ya kupokea kijiti hicho,  Samia alikuwa makamu wa Rais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania,  Rais akifia madarakani,  makamu wa Rais huapishwa kuwa Rais.

“Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia.

 Wanawake bado hatujaweka Rais mwanamke, rais huyu amekaa kwa sababu ya kudra ya Mungu na matakwa ya katiba,  tulichochangia sisi na dada zetu na mama zetu ni ile kusukuma hadi mwanamke akawa makamu wa Rais ule ndio mchango mkubwa tulioufanya wanawake, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, " amesema kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Septemba 15, 2021  alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya demokrasia dunia.

“Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameaanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia."

Advertisement

“Fadhila za Mungu zikija mikononi kwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu ndugu zangu wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hizi, wanawake tumefanaya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hizi, tumebeba sana wanaume  katika siasa za nchi hizi leo Mungu ametupa baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani."

Advertisement