Sekta ya misitu, chai yaipatia Iringa Sh4 trilioni kwa mwaka

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema zaidi ya asilimia 75 ya pato la Mkoa humo linatokana na sekta ya  misitu pamoja na zao ya chai ambapo kwa wastani Sh4 trilioni kwa mwaka zinakusanywa.

Mufindi. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema zaidi ya asilimia 75 ya pato la Mkoa humo linatokana na sekta ya  misitu pamoja na zao ya chai ambapo kwa wastani Sh4 trilioni kwa mwaka zinakusanywa.
Dendego ameyasema hayo leo Jumanne 22, 2023, wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa misitu kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani hapa.

Aidha Dendego amesema sekta ya misitu na kilimo cha chai katika mkoa huo limekuwa na fursa kubwa  kuongeza pato ambapo kwa wastani Sh4 Trioni kwa mwaka zinakusanywa kupitia sekta hizo huku mwananchi mmoja mmoja akipata Sh4.08 milioni kwa mwaka.
Amesema kuwa sekta hiyo ni lazima  itumike nguvu kubwa kutokana na inapaswa kutazamwa kwa  jicho la kipekee. Hivyo ni wajibu kama kiongozi wa serikali kuhakikisha sekta zote zinapewa kipaumbe kwa kukaa na wadau na kitathmini mafanikio na kuzifanyia kazi changamoto zinapotatikana.

Dendego amesema lengo la kikao hicho  ni kwa ajili ya kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya misitu na kuzitambua na kuweka mikakati ya kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.
" Lengo la kikao hiki ni kutambua na kuhakikisha tunaweka mipango madhubuti ya kuimarisha na kukuza sekta ya misitu kwa wakulima wadogo wadogo hadi ngazi ya juu kuwa maslahi mapana ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Dendego.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoani hapa, Mhandisi Leornad Massanja amesema kuwa  katika ushindani wa kibiashara na uchumi ni lazima wawepo   kwenye ushindani huo.
" Kama mnavyofahamu duania ipo katika mchakato wa ushindani wa kibiashara na kiuchumi hivyo maandalizi makubwa yanatakiwa kupitia vikao kama hivi ili kueleza changamoto zilizopo katika ushindani huo," amesema Mhandisi Massanja.