Selcom: Kujenga uwezo ili kukuza ujumuishaji katika ubunifu

Kodi mpya za digitali: Mtihani kwa uchumi

Muktasari:

  • Kukiwa na maendeleo ya kasi ya ikolojia ya ubunifu, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kuwa mshiriki muhimu katika uchumi wa kidigitali duniani, hasa kutokana na juhudi za ukuaji wake katika sekta ya huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na malipo ya kidigitali.

Dar es Salaam. Kukiwa na maendeleo ya kasi ya ikolojia ya ubunifu, Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kuwa mshiriki muhimu katika uchumi wa kidigitali duniani, hasa kutokana na juhudi za ukuaji wake katika sekta ya huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na malipo ya kidigitali.


Wakati hili lilikuwa na faida ya moja kwa moja kwa kampuni kadhaa katika masuluhisho ya kidigitali ndani ya nchi, kuna mahitaji yanayoongezeka ya kazi za stadi za juu zinazohusiana moja kwa moja na sekta za biashara ya kidigitali, ujasiriamali wa kidigitali na biashara ya kimtandao (e-commerce). Selcom, kama mtoaji mkubwa wa huduma za kifedha na malipo, imekuwa ikiongoza katika kufanya malengo hayo yote yaende sambamba kwa kutumia bidhaa zake sokoni.


Katika mahojiano na The Citizen, ofisa mkuu wa mikakati, Rushika Pattni alieleza ni jinsi gani kampuni iliweka kipaumbele katika ujumuishaji wa kidigitali kwa kuanzisha programu za kukuza stadi za vijana na ubunifu.

Kuanzia kufanya kambi kwa ajili ya kufungua uwezo wa kufikia APIs, Selcom imeendelea na kasi ya kufanya malipo kuwa rasmi na kufanya utatuzi wa changamoto kuwa wa kidigitali kwa kuruhusu bidhaa zake za sasa kupatikana kwa kutumia ujumuishaji wa API kwa ajili ya biashara zinazotaka kwenda kidigitali.

Selcom: Kujenga uwezo ili kukuza ujumuishaji katika ubunifu


“Kwa kuwa na ujuzi wa kiteknolojia na uzoefu, awali, tulifanya kazi moja kwa moja na SME (kampuni ndogo na za ukubwa wa kati) na mashirika makubwa, hivyo kuunganisha zaidi ya biashara 50,000 katika kufanya malipo kuwa ya kidigitali kwa kutumia jukwaa letu la wafanyabiashara, yaani Selcom Pay,” alisema.


Hata hivyo, kutokana na kubadilisha mikakati wakati wa janga la virusi vya corona, Selcom ilibaini ongezeko la mahitaji ya kujumuisha malipo yaliyotolewa na majukwaa ya upande wa tatu au fintechs, teknolojia zinazowezesha huduma za kifedha na kibenki.

Fintech na majukwaa mengine ya upande wa tatu yakaanza kutengeneza bidhaa nyingine za kutatua matatizo na kama huduma za kuongeza thamani ndani ya sekta kama vile usimamizi wa usafirishaji na hata kufanya burudani kuwa za kidigitali.


Mara zote lengo la Selcom lilikuwa ni kuwa mwezeshaji na kusaidia kusukuma mbele ajenda ya taifa kwa pamoja na wadau wote, licha ya kwamba wanachukuliwa kuwa washindani katika maana ya kawaida.
Kambi zilisaidia kutoa nafasi na majukwaa kwa kampuni tofauti na kutumia API ya Selcom kwa bidhaa zao au program tumishi, na muhimu kusukuma bidhaa zao wenyewe kwa manufaa ya mtumiaji wa mwisho.

Hii inajumuisha bidhaa za Selcom ambazo ni utoaji ankara, e-commerce, APIs za malipo, na nyingine ambazo zinatumiwa na kampuni kwa pamoja.

Kupunguza muda wa matumizi kutoka kuufanya mnyororo wa thamani kuwa wa kidigitali katika biashara ya majengo na dawa, hadi jinsi ya kukopa na zaidi. Lengo la Selcom na kuwa na uwazi na kuchangia ujuzi ili kuwezesha ubunifu kwa wengine bila ya kujali ukubwa wao au uzoefu kama biashara.


Kazi haikuishia hapo, anaongeza Rushika, Selcom ililazimika pia kuunda upya muundo wake wa kwa ajili ya kunoa vipaji ambavyo vinaweza kusaidia kirahisi wateja kwenda kidigitali. Wakati ndani ya Selcom, wana vifaa na wamepata mafunzo ya bidhaa tofauti na mahitaji ya kiufundi kuanzia siku ya kwanza, mpango wa kampuni ni kutumia tija na ubunifu wa vijana ili, kutokana na mabadiliko ya baadaye, kuwe na ushirikiano baina ya wajasiriamali vijana wenye mawazo yanayofanana katika kutatua changamoto zilizopo sasa Tanzania.”


Mwishoni, lengo la Selcom ni kuhakikisha kama changamoto ni kwenda kidigitali na kufanya malipo yawe ya kidigitali katika maeneo muhimu sana, basi kusiwepo na kitu cha kukwamisha.