Serikali ya Tanzania yaeleza mipango kufufua zao la kahawa Kilimanjaro

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akijibu maswali bungeni katika kikao cha 27 cha mkutano wa Bunge la Bajeti, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kufufua zao la kahawa mkoani Kilimanjaro, Bunge limeelezwa leo Jumanne Mei 11, 2021.

Dodoma. Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kufufua zao la kahawa mkoani Kilimanjaro, Bunge limeelezwa leo Jumanne Mei 11, 2021.

Naibu Waziri wa Kilimo,  Hussein Bashe amesema hatua hizo zinatokana na kushuka kwa uzalishaji kutoka tani 3,486 mwaka 2014/15 hadi kufikia tani 1,428 mwaka 2020/21 sawa na asilimia 59.

Bashe alikuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Hai (CCM), Saashisha Mafuwe aliyetaka kujua kama Serikali haioni ni wakati sahihi wa kufufua zao hilo wilayani Hai.

Katika maelezo yake Bashe amesema kushuka huko kumechangiwa na baadhi ya wakulima kuacha kuyahudumia mashamba kutokana na kuzorota kwa uliokuwa mhimili wa uzalishaji wa kahawa mkoani Kilimanjaro.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha ukame na kukosekana kwa maji ya umwagiliaji.

Amebainisha kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kufufua zao hilo mkoani Kilimanjaro  kwa kukifufua na kukijenga upya chama kikuu cha ushirika wa kahawa Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU).

Nyingine ni kurejesha mali zilizouzwa kiholela na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha ubadhilifu wa mali za ushirika.

T: Serikali ya Tanzania yaeleza mipango kufufua zao la kahawa Kilimanjaro

S: Serikali imeshaanza kuchukua hatua za kufufua zao la kahawa mkoani Kilimanjaro, Bunge limeelezwa leo Jumanne Mei 11, 2021.

Habel Chidawali, Mwananchi