Serikali yaeleza ilivyodhibiti sukari kuingia Tanzania kiholela

Tuesday February 16 2021
sukaripicc
By Mwandishi Wetu

Mvomero. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Aldof Mkenda amesema Serikali imejitahidi kuziba mianya ya sukari kuingia kiholela Tanzania.

Profesa  Mkenda amesema hayo leo Jumanne Februari  16, 2021 katika Kiwanda cha sukari cha Mtibwa wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Amesema kutokana na hali hiyo  Serikali imepunguza pengo la  uhaba wa sukari na kufika tani kati ya Sh40,000 na 50,000 kwa mwaka.

Profesa  Mkenda amesema kwa miaka mitano Serikali imelinda sekta ya sukari nchini.

Hata hivyo, amewataka wawekezaji kuongeza uzalishaji wa sukari  nchini huku akishauri kuwepo

viwanda vidogo vya sukari nchini ili wakulima wa miwa wauze na wasitegemee mwekezaji mmoja.

Advertisement

"Watanzania njooni muwekeze kwenye sukari, kuna fursa huku Serikali itawashika mkono. Benki zipo zinatoa mikopo. Kule  Kilombero miwa 300,000 imetupwa kwa kukosa soko, sawa na tani 35,000 za sukari,” amesema.

Hata hivyo, mkulima Seif Sekiloje amesema wakulima wa miwa hawana mtetezi licha  ya kuwapo vyama vya ushirika.

Advertisement