Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yafunga maabara tembezi ya Ebola Kagera

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk Issessanda Kaniki

Muktasari:

  •  Katika juhudi za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini, Serikali imeweka maabara tembezi ya kupima virus vya ugonjwa huo katika kituo cha afya Kabyaire kilichopo wilaya ya Misenyi mkoani humo.


Bukoba. Katika juhudi za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini, Serikali imeweka maabara tembezi ya kupima virus vya ugonjwa huo katika kituo cha afya Kabyaire kilichopo wilaya ya Misenyi mkoani humo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk Issessanda Kaniki akiongea na Mwananchi Digital baada ya kikao na wadau wa afya dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huo kilichofanyika leo Jumamosi Oktoba Mosi, 2022 amesema maabara hiyo itarahisisha upimaji.

“Mashine iliyofungwa kituo cha afya Kabyaire baada ya mtu kupimwa virus vya ebola majibu yanatoka ndani ya masaa mawili na wameletwa wataalamu wa afya wanne katika kituo hicho,” amesema Dk Kaniki.

Aidha ameeleza kwamba, mkoa huo umetenga hospitali 12 ambazo zitakuwa zinatoa matibabu ya ebola kwa atakayegundulika na yametengwa maeneo maalum kwa ajili ya kuweka wagonjwa wa ebola vituo vyote vya afya mkoani humo baada ya kuwapima na kuonekana na dalili litakuwepo gari la wagonjwa kwa ajili ya kuwasafirisha kwenye vituo maalum.

Amesema kila halmashauri wametenga eneo la karantini kwa ajili ya kuwaweka wahisiwa wa ebola, wale watakaobainika.

Naye Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha elimu ya afya kwa umma, Dk Ama Kasangala amesema, hawewezi kufunga mpaka kati ya Tanzania na Uganda, kwani kuna shughuli zizonaendelea za uzalishaji kwa wananchi badala yake watajikita katika kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na virusi hivyo.

Ametaja njia za kujikinga kuwa ni pamoja na kunawa mikono na maji ya sabuni au kutumia vitakasa mikono na kuepuka kusafiri na safari zisizo za lazima katika nchi zenye wagonjwa wa ebola.