Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaingilia kati mgomo wa madereva daladala Himo

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava akizungumza na madereva daladala na bajaji eneo la Njia panda ya mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi.

Muktasari:

  • Mgomo huo ambao umedumu kwa zaidi ya saa tano umetokea leo Februari 25, 2026 katika eneo la Njia panda, Mji mdogo wa Himo.

Moshi. Madereva daladala eneo la Njia Panda, Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, waligoma kwa zaidi ya saa tano wakidai madereva bajaji kuwanyang’anya abiria katika vituo vyao vya kupakia na kushusha abiria barabara ya Marangu–Mwika.

Mgomo huo ulitokea Februari 25, 2026 na kusababisha usumbufu kwa wasafiri, huku daladala zikisitisha huduma zikishinikiza bajaji kuondoka katika eneo lao. Hali hiyo ililazimu Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, kuingilia kati.

DC Mnzava aliwaagiza madereva bajaji kurejea katika eneo lao la awali la Bavaria ili kuondoa mwingiliano huo, huku akiwataka madereva daladala kuendelea na kazi ili kuepusha adha kwa wananchi. Pia alisisitiza kuitishwa kikao cha pamoja cha wadau, wakiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) na Polisi wa Usalama Barabarani, kutafuta suluhu ya kudumu.

Kwa upande wa daladala, Katibu wa Umoja wa Madereva Moshi–Marangu, Venance Minja, amesema kumekuwa na sintofahamu kuhusu mipaka ya shughuli za kila upande, akidai bajaji kufanya kazi kama daladala jambo linalozua msuguano.

Naye mwakilishi wa madereva bajaji Himo, Peter Mjema, amesema wanakabiliwa na changamoto ya kukosa kituo rafiki cha kupaki, hali iliyowalazimu kusogea karibu na eneo la daladala, akisisitiza kuwa wako tayari kwa mazungumzo ili kupata mwafaka.