Serikali yaitaka HELSB kuondoa adhabu ya asilimia 10 kwa wanaochelewesha mikopo

Tuesday May 04 2021
mikopic

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

By Sharon Sauwa

Dodoma. Serikali ya Tanzania imeagiza bodi ya wakurugenzi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuondoa adhabu ya asilimia 10 ya mkopo inayotozwa kwa wanufaika wanaochelewesha kulipa mikopo hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Mei 4, 2021 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan  katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza kufuta tozo ya asilimia sita ya mikopo inayotolewa na bodi hiyo.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, Profesa Ndalichako amesema Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo, itaondolewa kuanzia Julai Mosi  2021.

Amesema Serikali inaiagiza bodi ya HESLB kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo.

Advertisement