Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yatoa tahadhari ugonjwa wa silikosisi, 40 wakilazwa Kibong'oto

Naibu Waziri wa afya, Dk Florence Samizi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika hospitali ya Kibong'oto, wakati Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba alipokwenda kuweka jiwe la msingi katika jengo la utawala linalojengwa hospitalini hapo. Picha na Omben Daniel

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa afya, Dk Florence Samizi amesema ugonjwa huo hauna tiba na mgonjwa hupumulia oksijeni mpaka kufa kwake, hivyo akawataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa juu ya ugonjwa huo.

Siha. Serikali imewataka wachimbaji wa madini nchini kuchukua tahadhari madhubuti za kujikinga na ugonjwa wa silikosisi unaoathiri  mfumo wa upumuaji, kutokana na vumbi linalosababishwa  na shughuli za uchimbaji wa madini na mchanga.

Mpaka sasa zaidi ya watu  40 wanaosumbuliwa na  ugonjwa huo wamelazwa katika Hospitali maalumu ya Taifa ya magonjwa ambukizi Kibong'oto, Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro wakipumulia mashine ya oksijeni, ambapo watalazimika kutumia oksijeni hiyo mpaka kufa kwao.

Akizungumza leo Februari 21, 2026  na wananachi mara baada ya kuwekwa  jiwe la msingi jengo la utawala la hospitali hiyo na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa afya, Dk Florence Samizi  amewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kwa kuwa ni ugonjwa ambao hauna tiba.

 "Hapa kibong'oto tuna wagonjwa zaidi ya 40 ambao wana silikosisi, ugonjwa huu hauna tiba na ukishaupata huwezi kupumua. Kwa  hiyo wapo hapa Kibong'oto wakiendelea kutumia oksijeni na watatumia mpaka kufa,  ugonjwa huu hauna tiba," amesema Dk Samizi.

Amesema; "Niwaombe wachimbaji wote wa madini wachukue tahadhari ya kujikinga na vumbi wanapokwemda kwenye migodi maana ukishapata ugonjwa huo hauna tiba."

Pamoja na  mambo mengine Dk Samizi amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 inatokomeza ugonjwa wa kifua kikuu nchini na kuwa na Taifa  lenye afya bora.

Aidha, amesema tafiti zinazofanywa na hospitali hiyo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza muda wa matibabu kutoka matibabu sugu kwa mwaka mmoja hadi miezi sita.

"Tuna maabara inayotembea  na hii inatusaidia tunawapata wagonjwa kule kwenye jamii,  tunaamini huko ndio kuna wagonjwa wengi, lakini kule migodini, kwenye vijiwe, mikusanyiko ya watu  tuweze kuwagundua  mapema ili waweze kupata matibabu," amesema.

Dk Samizi amesema, hospital hiyo imepokea zaidi ya Sh32 bilioni kuhakikisha kwamba wanatokomeza ugonjwa wa kifua kikuu pamoja na kuboresha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Leonard Subi, amesema sasa hivi wapo katika hatua za mwisho ya  hospitali hiyo kuwa taassi ya Tanzania ya magonjwa ya kuambukiza ambayo itakuwa na Sheria zake.

"Hospital yetu hii ni moja ya mikakati ya Serikali ya mapambano ya magonjwa haya ambayo yanasababishwa na  milipuko, tuna imani huku tunakoendelea tunaenda kuzuri lengo letu kubwa, ni kuwa taasisi bora ya Kimataifa ya udhibiti na mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza," amesema Dk Subi.

Aidha, amesema ili kuboresha huduma za afya kwenye masuala ya tafiti kila mwaka wanafanya machapisho 10 na mpaka sasa wamechapisha machapisho mbalimbali 140.

"Tafiti za matokeo haya ni kushiriki kwenye kupunguza muda wa matibabu sugu ya kifua kikuu kutoka miaka miwili hadi miezi tisa na sasa tumeenda miezi Sita," amesema Dk Subi.


Dk Mwigulu awapongeza Kibong'oto

Akizungumza na wananachi katika viwanja vya hospitali hiyo, Dk Mwigulu Nchemba ameipongeza hospitali hiyo kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali pamoja na utoaji mzuri wa huduma za afya.

"Nawapongeza sana kwa kazi hii ambayo imefanyika vizuri hapa, nimekagua na nimeridhika na hatua ambazo zimefanyika hapa, taarifa zetu za ulinzi na usalama inaonyesha kazi inaenda vizuri, hongereni sana," amesema Dk Mwigulu.