Sh2.8 trilioni za usajili kuongeza msisimko England

Thursday August 04 2022
englandpiic
By Mwandishi Wetu

Manchester, Uingereza (AFP). Klabu za Ligi Kuu ya England zimetumia dola bilioni 1.2 za Kimarekani katika kunasa wachezaji kipindi hiki cha joto kabla ya kuanza msimu mpya Ijumaa, lakini mabingwa Manchester City wanaonekana wataendeleza ubabe.

Baada ya kutwaa ubingwa mara nne katika miaka mitano, kikosi cha Pep Guardiola kimeimarishwa na kuwasili kwa jina kubwa katika majira ya joto la Erling Haaland.

Mshambuliaji huyo raia wa Norway alikuwa na fursa la kuchagua klabu anayoitaka baada ya kutikisa mabao mara 85 katika mechi 88 alizoichezea Borussia Dortmund na kufuata nyayo za baba yake Alf Inge-- nahodha wa zamani wa City -- kwenda rangi ya bluu jijini Manchester.

Haaland, aliyenunuliwa kwa pauni milioni 51 za Kiingereza (sawa na Sh 145.1 bilioni za Kitanzania) anaweza kulazimika kusahau mechi yake ya kwanza ambayo alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao mwishoni mwa mchezo wa Ngao ya Hisani ambayo City walilala kwa mabao  3-1 mbele ya Liverpool Jumamosi, lakini Guardiola alionya kuwa wanaodhihaki ufalme wa timu yake akisema "mabao yatakuja". (Pauni moja ya Kiingereza ni sawa na Sh2,800 za Kitanzania)

"Hakuna sababu ya kutojiamini," alisema Guardiola. "Walichokifanya hawa vijana, si tu kwenye Ligi Kuu, lakini hata kwenye mtoano, hatua tulizopiga Ulaya na katika mambo mengi."

Katika dirisha lenye mabadiliko makubwa Etihad, mshambuliaji Muargentina Julian Alvarez, aliyenunuliwa kwa pauni milioni 14 za Kiingereza, na kiungo wa kimataifa wa England, Kalvin Phillips (pauni milioni 42) pia wamewasili klabuni hapo.

Advertisement

Lakini Guardiola aliruhusu wachezaji kadhaa wazoefu kuondoka na kujiunga na wapinzani wao, huku Gabriel Jesus, aliyenunuliwa kwa pauni milioni 45 za Kiingereza, na Oleksandr Zinchenko (pauni milioni 32) wakitua Arsenal na Raheem Sterling akijiunga Chelsea kwa ada ya pauni milioni 47.3.

Liverpool imejiweka vizuri kutumia makosa yoyote yatakayotokana na kuporomoka kwa ubora wa City.

Timu ya Jurgen Klopp walinyimwa nafasi ya kihistoria ya kutwaa vikombe vinne kwa tofauti ndogo msimu uliopita baada ya kuzidiwa na City kwa tofauti ya pointi moja, na kufungwa

bao 1-0 na Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutwaa vikombe vya FA na Kombe la Ligi.

Wekundu hao pia wamehuisha safu yao ya ushambuliaji kwa kumnunua Darwin Nunez kwa ada iliyoweka rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 85 ili azibe nafasi ya Sadio Mane ambaye amejiunga Bayern Munich.

Nunez alionyesha makali yake mapema katika Ngao ya Jamii, akisababisha penati na kufunga bao na kuiwezesha Liverpool kushinda mwishoni mwa mechi hiyo.

Changamoto ya Tottenham katika ubingwa?

City na Liverpool zimetawala soka nchini England kwa miaka mitano iliyopita, lakini kama kuna changamoto yoyote, basi inaweza kuwa inatoka Tottenham.

Kabla ya msimu kamili wa kwanza wa Antonio Conte akiwa kocha wa klabu hiyoe, Mtaliano huyo amekuwa akiungwa mkono na bodi baada ya kuwanunua Richarlison (pauni milioni 50), Yves Bissouma pauni milioni 25), Ivan Perisic, Djed Spence, Clement Lenglet na Fraser Forster.

Muhimu pia, Tottenham pia imewabakiza nyota wake wawili, Harry Kane na Son Heung-min wakati wakipania kutwaa taji la kwanza la ligi katika miaka 62.

Arsenal imekuwa iking'aa katika mechi za kujiandaa kwa msimu, huku Jesus akiwa moto

katika mechi ambazo timu hiyo ilizisambaratisha Chelsea na Sevilla. Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel aliilaumu timu yake "kw akutokuwa shindani" baada ya

kuchapwa mabao 4-0 na Arsenal jijini Orlando ana klabu hiyo iko katika kipindi cha mpito baada ya kununuliwa na Todd Boehly.

Pia kuna kazi kubwa kwa kocha mpya wa Manchester United, Erik ten Hag huku hali ya baadaye ya Cristiano Ronaldo ikiwa haijulikani kama atabakia kwa Mashetani Wekundu.

Nedwcastle mpya yavuka matumizi

Huku kiwango cha fedha za kununulia wachezaji kikiwa kikubwa, cha kustaajabisha ni ukimya wa Newcastle tangu inunuliwe na mfumo wa serikali ya Saudi Arabia.

Newcastle imetumia chini ya pauni milioni 60 kumnunua beki Mholanzi, Sven Botman, kipa wa England Nick Pope na kumpa mkataba beki wa kushoto, Matt Targett.

Vijana wapya Nottingham Forest wametumia pauni milioni 70 kusajili wachezaji 12 kwa ajili ya msimu wa kwanza katika miaka 23 kwenye ligi ya juu kwa timu hiyo ambayo ishawahi kutwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili.

Kiwango hicho hakijumuishi hata mkataba wa mwaka mmoja wa Jesse Lingard unaoripotiwa kufikia mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki baada ya kujiunga bila ya ada akitokea Manchester United.

Advertisement