Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh2 bilioni kujenga barabara Mbeya Vijijini, Mbunge Njeza atoa neno

Muktasari:

  • Kutokana na changamoto ya ubovu wa barabara inayowakabili wananchi wa Kata za Shizuvi na Ilembo, Tarafa ya Isangati Jimbo la Mbeya Vijijini katika kusafirisha mazao na bidhaa mbalimbali, Serikali imesaini mikataba miwili na makandarasi kwa ajili ya kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe ikiwemo Barabara ya Sapanda Isonso Ilembo.

Mbeya. Wiki moja baada ya wabunge kuiomba Serikali kuangalia namna ya kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutokana na kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini, Serikali imetenga Sh2 bilioni ujenzi wa barabara Mbeya Vijijini.

Kutokana na changamoto ya ubovu wa barabara inayowakabili wananchi wa Kata za Shizuvi na Ilembo, Tarafa ya Isangati Jimbo la Mbeya Vijijini katika kusafirisha mazao na bidhaa mbalimbali, Serikali imesaini mikataba miwili na makandarasi kwa ajili ya kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe ikiwemo Barabara ya Sapanda Isonso Ilembo.

Wananchi wa kata hizo sasa wana matumaini mpaya kutokana na mpango wa Serikali kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe kama ilivyoelezwa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na vijijini (Tarura) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Alberto Kindole kuwa barabara hizo zitagharimu zaidi ya Sh2 bilioni.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi wa Kata za Shizuvi na Ilembo kwenye shughuli ya utiaji saini na wakandarasi, meneja huyo wa Tarura Mkoa wa Mbeya ameeleza kuwa barabara za vijijini ni muhimu na zinasaidia katika usafirishaji hasa wa mazao mbalimbali kama ilivyoombwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini na madiwani kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na wananchi hao, Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza amesema wananchi wake wana uhitaji mkubwa wa barabara utakaowasaidia katika usafirishaji mazao na wagonjwa ikizingatiwa kuwa eneo hilo ni wazalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo mbao, pareto na viazi.

Pamoja na hayo, Mbunge Njeza ameishukuru Serikali kwa uidhinishaji fedha zaidi ya Sh2 bilioni na kwa ajili ya barabara mbili.

Barabara zilizosainiwa mikataba yake kwa ajili ya kuanza ujenzi ni za Ilembo Mwala na ile ya Sapanda Ilembo Isonso ambazo zote zitaanza ujenzi wake rasmi mwanzoni mwa mwezi Juni 2025 na zitajengwa kwa kiwango cha changarawe kwa muda wa miezi nane.