Sh2 bilioni kuwapelekea maji wananchi 16,600 Korogwe

Meneja wa Wakala wa maji vijijini na usafi wa mazingira (RUWASA),  Mhandisi Upendo Omari akisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji katika vijiji saba Wilayani Korogwe.

Muktasari:

Zaidi ya wananchi 16,600 waliopo kwenye vijiji saba katika Halimashauri ya  wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya serikali kuwapelekea miradi ya maji mitatu yenye thamani ya Sh 2 bilioni.

Korogwe. Zaidi ya wananchi 16,600 waliopo kwenye vijiji saba katika Halimashauri ya  wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya serikali kuwapelekea miradi ya maji mitatu yenye thamani ya Sh 2 bilioni.

Wakiongea mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa miradi hiyo baina ya wakandarasi wataojenga pamoja na Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijiji Ruwasa mkoani hapa.

Mmoja wa wananchi hao waliipongeza serikali Kwa uamuzi wake busara wa kuwapelekea huduma hiyo ambayo Kwa Sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

"Hii ni mara ya kwanza sisi wanakijiji kuweza kushuhudia zoezi hili hii inaonyesha kuwa serikali hii inawajibika Kwa Wananchi hivyo tunaimani muda sio mrefu kazi ya utekelezaji inakwenda kuanza"amesema Ramadhan Mangare

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo amesema kuwa Miradi hiyo yote itatekelezwa ndani ya kipindi cha miezi sita na itakapokamilika itaongeza Hali ya upatikanaji wa maji kutoka asilimia 63.6 hadi kufikia asilimia 70.4.