Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh600 milioni kujenga sekondari mpya Hai

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe akichimba msingi katika shule mpya ambayo inajengwa katika kata ya Mnadani Wilayani Hai .Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Serikali imetoa Sh600 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Mnadani wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wanaoishi katika kata hiyo.

Hai. Serikali imetoa Sh600 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Mnadani wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi wanaoishi katika kata hiyo.

Wanafunzi wa kata hiyo wamekuwa wakitembea zaidi ya kilomita 30 kwa siku hali ambayo imewafanya baadhi yao kushindwa kumaliza masomo yao kutokana na umbali.

Akizungumza wakati wa kuchimba msingi wa shule hiyo, Mbunge wa jimbo hilo, Saashisha Mafuwe amesema ujenzi wa shule hiyo utakamilika ndani ya miezi sita.

"Serikali imetoa Sh600 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari mpya kwenye hii kata, mpaka sasa tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti Sh447 milioni na ujenzi huu utakamilika ndani ya miezi 6 kuanzia sasa," amesema Saashisha.

Pamoja na kukamilika kwa shule hiyo, amesema baadhi ya shule zilizopo katika wilaya hiyo zaidi ya 13 ni chakavu na zimekaa kwa muda mrefu bila kukarabatiwa.

"Shule nyingi zilizopo katika Wilaya ya Hai zimejengwa tangu mwaka 1962 zimechaa na ziko hoi, tuna shule 13 ndani ya wilaya ya Hai ambazo zimechakaa,"amesema Saashisha

Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wameishukuru SerikalI kwa ujenzi wa shule hiyo na kusema sasa utoro kwa wanafunzi utapungua.

Mkazi wa Shirinjoro, Anna Swai amesema watoto wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na shule kuwa mbali hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa wanafunzi na kushindwa kufikia malengo yao.